Ulinzi, usalama waendelea kuimarishwa Katavi
11 April 2024, 12:36 am
“Baraza kuu la Waislamu wanaupongeza uongozi wa Mkuu wa Mkoa kwa kuhakikisha hali ya utulivu inaimarika“
Na Lilian Vicent-Katavi
Wananchi wa mkoa wa Katavi Wamehakikishiwa usalama wakati wa kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi kwa kuwa jeshi la polisi lipo imara katika kuimarisha ulinzi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ambaye pia ni Mgeni Rasmi katika hafla ya Iftari ilyoandaliwa na Jeshi la Polisi April 9 iliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Club Mkoani Katavi
Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu amesema kuwa wao kama Baraza kuu la Waislamu wanaupongeza Uongozi wa Mkuu wa Mkoa kwa kuhakikisha hali ya Utulivu inaimarika.
Nae kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa ameshukuru Ushirikiano unaotolewa na Wananchi katika kukomesha Matukio ya Kihalifu na kuwataka kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani hapa ili kutokomeza Matukio ya Kihalifu.