Migogoro ya Ndoa ,Wivu wa Kimapenzi Chanzo cha Matukio ya Ukatili Katavi
3 April 2024, 9:26 pm
picha na Mtandao
” Wanandoa wanapaswa kusuluhisha Migogoro ya ndoa kwa njia ya amani na kuripoti vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa katika mamlaka husika“
Na Lilian Vicent -Katavi
Hayo yameelezwa na Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Anyulumiye Longo wakati akizungumza na Mpanda Redio Fm na kuongeza kuwa Wanawake na Watoto ndio Wahanga wakubwa wa Matukio hayo
Imeelezwa kuwa Migogoro ya Ndoa na Wivu wa kimapenzi ni moja ya sababu zinazopelekea kuongezeka kwa matukio ya Mauaji katika jamii.
Sauti ya Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Anyulumiye Longo
Katika hatua nyingine amewataka Wanandoa kusuluhisha Migogoro ya ndoa kwa njia ya amani na kuripoti vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa katika mamlaka husika.
Sauti ya Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Anyulumiye Longo akiwahasa wanandoa kuripoti matukio ya ukatili
Kwa upande wao Wananchi wameeleza kuwa wivu wa kimapenzi na usaliti unapelekea kuibuka kwa matukio hayo.
Sauti za wananchi wakitoa maoni Mseto juu ya sababu za matukio ya ukatili na mauaji katika jamii
Jamii imeaswa kutoa taarifa za Matukio kama hayo kwa haraka ili kuthibiti kutokea kwa matendo hayo .