Vijana Mkoani Katavi wametakiwa kufanya kazi ili wajikwamue kiuchumi
3 April 2024, 1:02 pm
picha na Mtandao
“Ni muhimu vijana kushiriki katika kufanya kazi ili kusaidia kuondoa makundi ya kiharifu“
Na Veronika Mabwile -Katavi
Imeelezwa kuwa uwepo wa baadhi ya vijana wasioshiriki katika shughuli za Kiuchumi katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatokana kutokuelezwa madhara yatokanayo na kutokufanya kazi
Hayo yameelezwa na baadhi ya Wakazi wa Manispaa ya Mpanda wakati wakizungumza na Mpanda Redio Fm na kusema kuwa chanzo cha uwepo wa baadhi ya Vijana wasiowajibika katika shughuli za Kiuchumi inachangiwa na malezi katika familia.
Sauti za Wananchi manispaa ya Mpanda wakizungumza
Afisa Ustawi wa Jamii Anyurumie Longo amesema ni muhimu vijana kushiriki katika kufanya kazi ili kusaidia kuondoa makundi ya kiharifu
Sauti ya Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda
Uwepo wa Vijana wasioshiriki katika shughuli za kiuchumi unachangia kuwepo kwa makundi ya kiharifu katika jamii hivyo vijana wamehimizwa kufanya kazi za kujipatia kipato .