Wananchi Katavi watakiwa kuacha kuchukua mikopo umiza
9 February 2024, 2:29 pm
Wananchi wamehimizwa kujenga tabia ya kuchukua mikopo katika taasisi za kifedha zinazozingatia sheria na miongozo ya serikali zikiwemo benki ili kuepuka usumbufu wa mikopo umiza.
Na Veronica Mabwile-Katavi
Imeelezwa kuwa Uwepo wa Elimu ndogo juu ya madhara ya tokanayo na mikopo umiza kwa baadhi ya watu katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuendelea kuongezeka kwa mikopo hiyo .
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda wakati wakiongea na kituo hiki na kuiomba serikali kuongeza juhudi za utowaji wa elimu katika jamii ili kuondoa migogoro inayojitokeza kutokana na mikopo hiyo
Sauti ya Wananchi wakitoa maoni kuhusu elimu ya mikopo umiza.
Akiongea na kituo hiki kwa njia ya simu Afisa maendeleo Manispa ya Mpanda amewataka wananchi kuijenga tabia kUuchukua mikop katika tasisi za kifedha zinazo zingatia sheria na miongozo ya serikali zikiwemo benki ili kuepuka usumbufu wameokuwa wakipitia kwa mikopo umiza.
Sauti ya Afisa maendeleo akizungumza kuhusu wananchi kuchukua mikopo maeneo maalumu.
Mikopo umiza ni mikopo ambayo hutolewa kwa watu kinyume na viwango halali vilivyo wekwa na mamlaka husika hivyo kusababisha migogoro kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakishindwa masharti magumu ya mikopo hiyo.