Katavi: Wachimbaji waaswa kuchukua tahadhari migodini kipindi cha mvua
1 February 2024, 5:54 pm
“Kaimu kamanda Geofrey Mwambungu amesema kuwa kuna ajali nyingi hutokea katika maeneo ya Migodini kipindi cha mvua”. Picha na Gladness Richard.
Na Gladness Richard-Katavi
Wachimba wa madini mkoani Katavi wameshauliwa kuchukua tahadhali kabla hawajaingia kwenye Migodi katika kipindi hiki cha mvua ili wasidondokewe na kifusi.
Ushauli huo umetolewa na Mkaguzi wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Katavi kaimu kamanda Geofrey Mwambungu amesema kuwa kuna ajali nyingi hutokea katika maeneo ya Migodini kwani mvua zinaponyesha husababisha kuta za udongo hurainika na kusababisha kuanguka kwa migodi.
Sauti ya Mkaguzi wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Katavi kaimu kamanda Geofrey Mwambungu akitoa tahadhari kwa wachimbaji kuchukua tahadhari kipinddi cha mvua wanapokuwa Migodini
Kwa upande wao wachimbaji wa madini wamesema kuwa wanatumia mbinu mbalimbali kwa kufunga Kamba pindi wawapo kuwa Mashimoni na kuvaa kofia Ngumu.
Sauti ya Wachimbaji wakieleza juu ya tahadhari wanazochukua wanapokuwa Migodini.
Mwambungu ameongezea kwa kusema kuwa ni jukumu lao kama Jeshi la zimamoto na uwokoaji kuwasimamia, kuwakagua na kuhakikisha wachimbaji wanakuwa salama wakati waingiapo migodini.