Mpanda FM

Uelewa bado mdogo Katavi mradi wa BBT

24 July 2023, 10:09 am

KATAVI.

Wananchi na wakulima mkoani Katavi wameonesha kutokuwa na uelewa wowote kuhusiana na mradi wa serikali unaoratibiwa na Wizara ya Kilimo, mradi wa jenga leo kesho iliyo bora maarufu kama (BBT).

Wakizungumza na Mpanda Redio FM wameeleza kuwa ni vema serikali ikatoa elimu kwa umma pindi wanapotaka kuanzisha mradi wenye manufaa makubwa kwa vijana hasa kwenye sekta ya kilimo ili kuzikimbilia fursa zilizopo.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu afisa kilimo mkoa wa Katavi Farid Mtiru amesema kuwa mradi huo unaratibiwa na Wizara ya Kilimo hivyo ni vigumu kuwa na takwimu kamili za vijana walioenda kwenye mafunzo hayo kutoka mkoani Katavi licha kuwepo tayari heka elfu mbili kwa ajili ya mradi huo wa BBT.

Mradi wa jenga leo kesho iliyo bora umeanzishwa na Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuwapa vijana maarifa katika kilimo ili kuimarisha uwepo wa chakaula na soko la mazao mbalimbali ya kilimo nchini.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayakilimo