Mpanda FM

Miti Yapandwa Kituo cha Afya Kazima

20 March 2023, 5:05 pm

KATAVI

Wanawake wa kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania [KKKT ]na Wanawake wakatoliki wa Tanzania [WAWATA]jimbo la Mpanda wameeleza umuhimu wa utunzaji mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti.

Wameyasema hayo wakati wa zoezi la upandaji miti ambalo limefanywa na wanawake katika kituo cha afya Kazima ambapo wamesema lengo la kuungana na kufanya zoezi hilo ni kutambua umuhimu wa utunzaji wa mazingira ili kuepukana na madhira yanayoweza kutokana na uharibifu wa mazingira.

Mwenyekiti Idara ya wanawake KKKT jimbo la Mpanda Felister Chaula amesema ushirikiano na kujitoa kwa jamii haitakuwa mwisho huku akiomba miti hiyo kutunzwa ili kuboresha mazingira.

Kwa upande wake Mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda Haidary Sumry ambaye alikuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo amepongeza hatua zilizochukuliwa na muungano wa wanawake hao huku akisisitiza ushirikiano huo kudumu zaidi.