Mpanda FM

Watu Wenye Ulemavu Washauriwa Kuchangamkia Mikopo ya Halmashauri

9 March 2023, 1:12 pm

KATAVI

Watu Wenye ulemavu Mkoani Katavi  wameshauriwa  kuchangamkia fursa ya  mikopo ya asilimia mbili inayotolewa na serikali kupitia  halmashauri zote nchini.

Katibu wa Chama cha watu wenye ulemavu Mkoa wa Katavi  Godfrey Sadala ameiambia Mpanda Radio kuwa watu wenye ulemavu wanahofia kwenda kufuatilia fedha za Serikali kwa kuhofia marejesho  kuwataka kujitokeza kuomba mikopo hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya watu wenye ulemavu wamesema kuna changamoto ya ufuatiliaji wa mikopo hiyo na kuwashauri wenzao kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ili kujikwamua kiuchumi.

Katika Bajeti mpya ya Mwaka 2023/2024 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amezisisitiza Halmashauri Zote mkoani hapa kuendelea kutenga asilimia 10 kwa ajili ya mahitaji ya Vijana Wanawake na watu wenye Ulemavu.