Mbunge wa Mpanda Mjini Ataka Elimu kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini
4 March 2023, 5:49 pm
MPANDA
Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi ameitaka sekta ya madini mkoani Katavi kutoa ELimu ya kutambua maeneo ya njia ya mtandao, nukta majira kwa wachimbaji wadogo wa madini ili kuondoa migogoro ya maeneo iliyoanza kujitokeza kwa wachimbaji wageni .
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa amesema kumekua na changamoto ya utambuzi wa maeneo ikiwemo wachimbaji wa zamani kuchukuliwa maeneo yao na wageni Mara baada ya teknolojia Ya nukta majira Kutumika, Jambo ambalo Linaweza kuleta migogoro kwa wachimbaji hao.
Akijibu hoja hiyo afisa madini wa mkoa wa Katavi injinia Andrew Mwalugaja amesema changamoto ya wachimbaji wa madini mkoani hapa wengi wao Walikuwa wanatumia njia za asili ingawa wanatakiwa kukata leseni za kisasa ambazo zinatumia nukta majira jambo lililoleta ukakasi kwa wajumbe wa mkutano.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi ccm mkoa wa Katavi Iddy kimanta amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wachimbaji wa madini kuhusu sekta ya madini mkoani hapa na kumwomba mkuu wa mkoa kushughulikia changamoto hiyo ili kuwanusuru wachimbaji wa mkoa wa katavi.