Mpanda FM

Mgogoro wa Wachimbaji Dirifu, Mkuu wa Wilaya Ataka Subira.

4 March 2023, 1:54 pm

MPANDA
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewataka Wananchi na wachimbaji wa madini wa kijiji cha Dirifu kuwa na subira na kuishi kwa amani kufuatia mgogoro unaoendelea katika kijiji hicho.

Akitoa maelekezo hayo kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda, diwani wa kata ya Magamba Fortunatus Chiwanga amesema kuwa ofisi ya mkuu wa wilaya imewataka wananchi kuwa na utulivu na kutatua mgogoro kwa amani, ili kuepusha yale yanayoweza kujitokeza, pia kutengeneza mazingira mazuri kwa wachimbaji kwa kutafuta muwekezaji anaeweza kutengeneza mlima huo.

Kwa upande wa wanakijiji na wachimbaji katika kijiji cha Dirifu wamesema wanaheshimu maagizo na wapo tayari kuchangia gharama za kukata mlima ili kutengeneza mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo.

Katika hatua nyingine uongozi wa kikundi cha kagera group kupitia mwenyekiti wa kikundi hicho umesema kuwa umeshaingia makubaliano na muwekezaji na tayari ameanza kazi za awali za kutengeneza mlima kulingana na maelekezo waliyoyapata kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya.

Mkutano huo uliisha bila kuwa na muafaka baada ya wananchi na diwani wa kata ya Magamba kutaka taarifa ya maandishi na makubaliano ambayo Kagera group wameingia na muwekezaji na kuwatakakuleta taarifa hiyo katika mkutano mwingine ili kuyaweka wazi yaliyojadiliwa.