Zaidi ya Miti Millioni Mbili Inataraji Kupandwa Tanganyika
25 January 2023, 10:44 am
MPANDA
Jumla ya miti milioni mbili na elfu kumi na nne inatarajiwa kupandwa katika maeneo mbalimbali wilayani Tanganyika mkoani katavi.
Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya mpanda Jamila Yusufu wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika shule ya sekondari majalila ambapo amesema kuwa jukumu la upandaji miti na uhifadhi wa mazingira ni la kila mmoja.
Aidha amewataka wakala wa TFS na wakala wa maji vijijini RUWASA kupanda miti katika vyanzo vya maji na kuendelea kuhifadhi na kutunza mazingira huku akiwataka kuwachukulia hatua kali za kisheria wale ambao wanafanya shughuli zote za kibinadamu katika vyanzo vya maji
Kwa upande wake makamu mkuu wa shule ya sekondari majalila mwalimu Joseph munyonga ameahidi kushirikiana na jamii katika kuhakikisha wanapanda miti na kutunza mazingira.
Zoezi la upandaji miti katika mkoa wa katavi limeanza January 24 huku likitarajiwa kukamilika january 26 mwaka 2023.