Mpanda FM

Serikali iingilie kati kipindi cha mauzo ya Pamba

1 December 2022, 5:05 am

TANGANYIKA

Wakulima wa pamba wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi wameiomba serikali kipindi cha mauzo ya pamba kuingilia kati na kusimamia zoezi ili kuepusha sintofahamu ambayo huwa inajitokeza kwa baadhi ya maeneo watu kutokulipwa stahiki Zao.

Maombi hayo wameyatoa wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu alipotembelea na kukagua mashamba ya pamba na kutoa elimu kwa wakulima juu ya kilimo chenye tija.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu baada ya kukagua mashamba ya wakulima amesisitiza wakulima kuachana na kilimo cha kienyeji na wazingatie maelekezo ya wataalam.

Katibu wa chama cha ushirika cha Kamwendo AMCOS Method Madoshi amewataka wakulima kuongeza tija katika uzalishaji ili ushuru unaokatwa wakati wa mauzo ya pamba kupitia vyama vyao vya ushirika, utumike kuwakatia bima za afya na waweze kukopesheka na taasisi za kifedha.