Machinga Walia na Changamoto za Mikopo ya Halmashauri
15 September 2022, 10:06 pm
KATAVI
Wajasiliamali wadogo wadogo maarufu kama machinga Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamezungumzia changamoto wanazokutana nazo katika utoaji wa mikopo katika vikundi.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm, na kubainisha sababu zinazopelekea baadhi ya vikundi kutopata mikopo baada ya kujisajili , ni kutokana na kutokuwa waaminifu pale wanapopewa mikopo hiyo. .
.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la machinga Mkoa wa Katavi Marco Ernest, amesema kuwa ni wajibu wa kila kikundi kufuatilia uwezekano wa kupata mikopo baada ya kujisajili, na badala yake wasisubili kufuatwa kwaajili ya kupewa mikopo hiyo.
.
Nae Afisa Maendeleo Mkoani hapa Marietha Mrozi, amesema kuwa wapo tayari kusikiliza changamoto hizo na kuzitaftia ufumbuzi hivyo kuwataka wa machinga kufika ofisini .