Kizungumkuti Viwatilifu Vya Korosho
5 September 2022, 10:51 am
Wananchi wa kijiji cha Isinde kata ya Mtapenda Halimashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wamelalamikia kutopewa viwatilifu kwaajili ya zao la korosho licha ya kuwa wakulima wa zao hilo zaidi ya miaka mitano.
Wakizungumza na kituo hiki wakulima hao wamesema kuwa wanapohoji juu ya viwatilifu hivyo wamekuwa wakipokea kauli za vitisho kutoka kwa viongozi
.
Hamis Rashid mbogo ambae ni mwenyekiti wa kijiji cha Isinde amekiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na ameahidi kufuatilia suala hilo ili kuwapatia haki wakulima hao.
.
Mpanda radio imemtafuta Afisa kilimo mkoani hapa faridi Mtiru ambapo amebainisha kuwa wakulima ambao hawajapata viwatilifu hivyo wafike katika ofisi za vijiji kwaajili ya kujindikisha ili waweze kupata katika awamu nyingine.
.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko alikabidhi Jumla ya viwatilifu 921 kwa wakulima wazao la korosho mkoani hapa kupitia bodi ya korosho Tanzania.