Jamii FM

Wabunge Mtwara wazungumzia mafanikio ya serikali

21 November 2024, 16:03 pm

Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini Hassani Mtenga akielezea mafanikio ya serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassani kwenye uzinduzi wa kampeni jana November 20,2024(Picha na Musa Mtepa)

Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika November 27, 2024 kote nchini ambapo wenyeviti wa mitaa,vijiji na wajumbe wake watarajiwa kuchaguliwa na hivi sasa ni mchakato kwa wagombea wa vyama vya siasa kunadi sera kwa wananchi (Kampeni)ili waweze kuchaguliwa.

Na Musa Mtepa

Baadhi ya wabunge wa mkoa wa Mtwara wamezungumzia mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM), katika kipindi cha uongozi wake.

Wabunge hao wamezungumza katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika Novemba 20, 2024, kwenye viwanja vya shule ya msingi Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani, ambapo wameelezea maendeleo yaliyotekelezwa katika majimbo yao.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdala Dadi Chikota, ametaja baadhi ya miradi inayotekelezwa katika jimbo lake, ikiwa ni pamoja na ukarabati wa mradi wa maji wa Mnyawi, ambapo zaidi ya bilioni 5.6 zimetumika.

Ameongeza kuwa kuna miradi mingine ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya na miundombinu, ambayo ina manufaa kwa wananchi wa Nanyamba.

Sauti ya Abdala Dadi Chikota Mbunge wa Jimbo la Nanyamba

Kwa upande mwingine, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmad Katani, ameelezea mafanikio yaliyofikiwa katika wilaya ya Tandahimba katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia  huku akiwahimiza wananchi wa wilaya hiyo kuchagua viongozi wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na maendeleo hayo.

Sauti ya Katani Ahmadi Katani Mbunge wa jimbo la Tandahimba

Mbunge wa Mtwara Mjini, Mh. Hassani Mtenga, kwa upande wake ametoa shukrani kwa Rais Samia na serikali yake kwa miradi mikubwa ya maendeleo iliyotekelezwa katika jimbo la Mtwara Mjini na kusema wananchi wa Mtwara wanajivunia miradi hiyo kutokana na manufaa ambayo sasa wanayaona katika jamii yao.

Sauti ya Hassani Mtenga Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini.