Jamii FM

Wazazi Wasisitizwa Kupeleka Watoto Shule mkoani Mtwara

15 October 2024, 22:30 pm

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala akizungumza na wananchi wa Chawi kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke aishiye kijijini(Picha na Musa Mtepa)

Siku ya Mwanamke anayeishi vijijini huadhimishwa October 15, ya kila Mwaka kwa lengo la kutambua mchango wa mwanamke anayeishi vijijini katika jitihada za kujiletea maendeleo yao na kuondokana na umasikini kiwa ni Pamoja na ushiriki wa kuinua Uchumi wa taifa,mtu binafsi na familia

Na Musa Mtepa

Wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule ili kupata elimu itakayowasaidia kukabiliana na fursa mbalimbali zinazojitokea mkoani Mtwara na kuepuka kuwa wasindikizaji wa fursa hizo.

Wito huu umetolewa leo, Oktoba 15, 2024, na mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, katika maadhimisho ya Siku ya Mwanamke aishiye kijijini yaliyofanyika katika Kijiji na kata ya  Chawi, halmashauri ya Mji Nanyamba.

Kanali Sawala ammesisitiza kwamba watoto wasiokuwa na elimu wataweza kuwa jamii inayolalamika, kwani fursa zote, iwe binafsi au katika sekta za umma, zinahitaji watu waliopata elimu.

Sauti ya 1 Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara

Aidha, ameongeza kuwa serikali inawatambua na kuwajali wanawake wanaoishi vijijini, na juhudi mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kuandaa mikakati ya kuwawezesha kielimu ili kuleta usawa wa kimaendeleo na amani nchini.

Sauti ya 2 Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara

Baltazar Komba, mwakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali la Baraza la Taifa (NACONGO), ametoa wito kwa maafisa wanaotoa mikopo kuzingatia vikundi vya wanawake wa vijijini, hasa wale wenye miradi inayokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Sauti ya Baltazar Komba Mwakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali Baraza la taifa (NACONGO)
Baltazar Komba Mwakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali Baraza la taifa (NACONGO)(Picha na Musa Mtepa)

Baadhi ya wanawake wa Kijiji cha Chawi wameeleza changamoto wanazokutana nazo, ikiwemo ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa wanaume katika kuwalea watoto na kutoshirikishwa katika matumizi ya fedha zinazopatikana kupitia kilimo cha zao la korosho.

Sauti ya wanawake wa Kijiji cha Chawi.