Jamii FM

Makala: Serikali na uboreshaji wa huduma ya afya ya mama mjamzito na watoto

6 June 2024, 15:18 pm

Wanafunzi wa shule ya Msingi Nanguruwe wakiwa kwenye michezo huku wamechanganyika na wanafunzi wengine walio na Mahitaji maalumu na wa kawaida. Picha na Gregory Millanzi

Na Gregory Millanzi na Mwanahamisi Chikambu

Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Mtwara waliwahi kulalamika kwenye makala zilizopita, kuhusu hali ya  utolewaji wa huduma bora ya afya ya mama mjamzito na mtoto kwenye vituo vya afya na Hospitali,  kuwa kuna baadhi wanadaiwa hela kwa ajili ya kuchangia huduma za afya.

Baada ya kusikia hayo, imepita miezi kadhaa tangu kutokea kwa changamoto hiyo ya Huduma ya Afya ya mama mjamzito na watoto chini ya miaka Mitano, Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imeamua kuja na suluhisho la mpango wa mama na mwana. ungana na Gregory Millanzi na Mwanahamis Chikambu kwenye simulizi ya makala haya.