Jamii FM

TARI Naliendele yatoa elimu ya uvunaji wa ufuta

16 May 2024, 17:46 pm

Joseph Mzunda mratibu wa programu ya zao ufuta kitaifa na mtafiti wa ufuta kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) Naliendele akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa elimu ya namna bora ya uvunaji wa ufuta kwa wakulima (Picha ni msaada wa wahisani)

Wakulima wanashukuru kupitia mbegu zinazozalishwa na kufanyiwa utafiti katika kituo cha Naliendele kwani wamekuwa wakipata tija kwenye uzalishaji hivyo wengine wanakaribishwa kufika na kujifunza namna bora ya uzalishaji wa zao la ufuta.

Na Musa Mtepa

Wakulima na wadau wa ufuta nchini wametakiwa kuzingatia ubora kwa kuanzia katika hatua za awali za kulima, uvunaji na utunzaji wa zao hilo ili kuendana na mahitaji ya soko linavyotaka.

 Hayo yamesemwa tarehe 15/5/2024 na mratibu wa programu ya utafiti wa ufuta kitaifa na mtafiti wa zao la ufuta kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) Naliendele Joseph Mzunda  wakati akitoa elimu ya jinsi na namna bora ya kulima na kuvuna  kwa baadhi ya wakulima  ambapo amesema kuwa wadau wa zao la ufuta lazima waangalie kuwa linapofika mikononi mwao lipo katika hali ya usafi ili kusitokee  lawama kutoka kwa wanunuzi.

Sauti ya 1 Joseph Mzunda mratibu wa program ya utafiti wa ufuta kitaifa na mtafiti wa zao la ufuta TARI Naliendele.

Aidha Bw  Mzunda ameseama kuwa wanunuzi wa ufuta wamekuwa na vigezo maalumu vinavyowafanya kununua ikiwepo ubora,rangi na Ladha yake huku akielezea  upekee unaopatikana kwenye ufuta unaozalishwa nchini ukilinganisha na nchi nyingine.

Sauti ya 2 Joseph Mzunda mratibu wa program ya utafiti wa ufuta kitaifa na mtafiti wa zao la ufuta TARI Naliendele.
Mtafiti wa zao la ufuta kutoka TARI Naliendele akitoa maelezo kwa wakulima namna bora ya kuvuna na kukausha ufuta

Hata hivyo Bw Joseph Mzunda amewataka wakulima kutunza kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua mbegu zilizokuwa bora na kwa ajili ya pembejeo na viuatilifu ili iwasaidie kutumia katika msimu unaofuata  wa kilimo cha ufuta

Sauti ya 3 Joseph Mzunda mratibu wa program ya utafiti wa ufuta kitaifa na mtafiti wa zao la ufuta TARI Naliendele.

Fatma Athumani na Aisha Wilson ni wakulima wa zao la ufuta kutoka kata ya Naliendele wamesema kupitia elimu waliyoipata kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) Naliendele itawasaidia katika kuandaa mashamba na namna bora ya kuvuna zao hilo tofauti na hapo awali walivyokuwa wakilima.

Sauti ya Fatma Athumani na Aisha Wilson wakulima wa zao la ufuta kutoka kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Ziada Athumani akielezea aliyojifunza kwa waandishi wa habari baada ya kutembelea shamba la ufuta la TARI Naliendele

Naye Ziada Athumani mkulima wa zao la ufuta kutoka kata ya Naliendele amesema lengo lake lilikuwa kupata elimu ya jinsi gani ya kulima ufuta kwa njia iliyokuwa bora ili aweze kupata tija hivyo kupitia TARI Naliendele amejifunza mengi kiwepo namna ya kupalilia na kuvuna kwake.

Sauti ya Ziada Athumani mkulima wa ufuta kutoka kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Wakulima wa ufuta wakionesha kwa vitendo namna bora ya kufunga na kukausha ufuta kwa njia iliyo bora