Jamii FM

Korosho ghafi tani 180,342 zauzwa ndani ya wiki tatu nchini

31 October 2024, 09:37 am

Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Frances Alfred akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa korosho(Picha na Grace Hamisi)

Hii ni katika kutolea ufafanuzi wa hali na mwenendo wa zao korosho katika msimu huu wa mwaka 2024/2024 ambao umeonesha uzalishaji kuwa mkubwa na bei rafiki kwa wakulima.

Na Grace Hamisi

Korosho ghafi tani 180,342 zimeuzwa kwa thamani ya bilioni 693 ndani ya wiki tatu, mara baada ya mnada wa kwanza kuanza tarehe 11 Oktoba 2024.

Ikiwa  ni ongezeko kubwa kwa msimu wa korosho wa mwaka 2024/2025, ikilinganishwa na tani 60,066 zilizouzwa katika msimu uliopita ndani ya kipindi hicho hicho.

Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Nchini (CBT), Francis Alfred, ameyasema hayo Oktoba 30,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa makosa na mauzo ya korosho nchini.

Sauti ya 1 Frances Alfred Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho ya Tanzani

Ameongeza kuwa ongezeko la uzalishaji pamoja na bei ya korosho kumeleta hamasa kwa wakulima wengi kupeleka korosho zao katika vyama vya msingi.

Sauti ya 2 Frances Alfred Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho ya Tanzani

Hata hivyo, bodi hiyo kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, inafanya jitihada za kuhakikisha mazao ya wakulima yanapatikana kwa urahisi.

Wanapata maelekezo na ushauri kutoka mamlaka za mkoa na wilaya ili kuhakikisha mizigo inayokwenda ghalani inatoka kwa haraka.

Sauti ya 3 Frances Alfred Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho ya Tanzani