Jamii FM

Makala ya matumizi ya mkaa

31 January 2026, 15:11 pm

Mmoja wa wajasiliamali akindaa jiko kwaajili ya kuchoma mahindi ili kupata kipato. Picha na Gregory Millanzi

Ongezeko la watu pamoja na kupanda kwa gharama za nishati mbadala kama gesi na umeme kumeongeza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa mkaa.

Na Gregory Millanzi

Kwa miongo mingi, mkaa umekuwa chanzo kikuu cha nishati kwa kaya nyingi, hususani katika maeneo ya mijini na vijijini. Hapo awali matumizi ya mkaa yalionekana kuwa suluhisho rahisi na la gharama nafuu kwa shughuli za kupikia na matumizi mengine ya kila siku. Wananchi waliutumia kwa kiasi na kwa uangalifu, wakitegemea misitu iliyokuwepo kwa wingi wakati huo.

Kadri miaka ilivyopita, ongezeko la watu pamoja na kupanda kwa gharama za nishati mbadala kama gesi na umeme kumeongeza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa mkaa. Hali hii imesababisha ukataji mkubwa wa miti kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa, jambo ambalo limeathiri vibaya misitu na mazingira kwa ujumla.

Athari za matumizi makubwa ya mkaa sasa zimeanza kujidhihirisha waziwazi. Miongoni mwa athari hizo ni uharibifu wa misitu, mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa joto duniani, pamoja na changamoto za kiafya zitokanazo na moshi unaozalishwa wakati wa matumizi ya mkaa majumbani.

Makala haya yanalenga kuelimisha jamii kuhusu madhara ya matumizi ya mkaa na kuhamasisha matumizi ya nishati safi, salama na endelevu ili kulinda mazingira pamoja na afya ya binadamu.

Bonyeza hapa kusikiliza kwa undani zaidi