Jamii FM

Makala ya Athari za ukataji miti

31 January 2026, 14:44 pm

Moja ya miti iliyokatwa katika mazingira. Picha na Gregory Millanzi

Athari za ukataji miti zinaonekana wazi kupitia ukame, mafuriko, na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri moja kwa moja maisha ya binadamu.

Na Gregory Millanzi

Ukataji miti umekuwa tatizo linalokua kwa kasi katika jamii nyingi, hasa maeneo ya vijijini. Hapo zamani, misitu ilikuwa chanzo muhimu cha mvua ya kutosha, hewa safi, na makazi ya wanyama pori. Wananchi waliitegemea misitu kwa mahitaji kama kuni, dawa za asili, na chakula, huku wakihifadhi mazingira yao.

Hata hivyo, kutokana na ongezeko la idadi ya watu pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya kilimo, makazi, na biashara ya mbao, ukataji miti umefanyika kiholela bila juhudi za kupanda miti upya. Matokeo yake yamekuwa makubwa na ya kutisha, yakiwemo kupungua kwa mvua, kuharibika kwa ardhi, kuongezeka kwa joto, pamoja na kutoweka kwa baadhi ya wanyama na mimea.

Kwa sasa, athari za ukataji miti zinaonekana wazi kupitia ukame, mafuriko, na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri moja kwa moja maisha ya binadamu. Simulizi hii inalenga kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa misitu na kuchukua hatua madhubuti za uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho.

Bonyeza hapa usikilize makala hii inayochambua kwa kina athari za ukataji miti mkoani Mtwara. Makala hii imeandaliwa na kusimuliwa na Gregory Millanzi.