Wasimamizi wasaidizi Mtwara DC wafundwa uchaguzi serikali za mitaa
30 September 2024, 14:58 pm
Na Musa Mtepa
Ndug. Abeid Abeid Kafunda, msimamizi wa uchaguzi, amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na kanuni ili kuepusha sintofahamu zinazoweza kujitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27,2024.
Wito huo ametolewa leo September 30,2024 wakati wa ufunguzi wa semina uliofanyika kwenye shule ya sekondari Mustafa Sabodo.
Kafunda amewataka wasimamizi wasaidizi wa ngazi ya kata na vijiji kuwa makini na kuzingatia mafunzo watakayopatiwa.
Shamimu Heri, msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Mayanga, ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kusimamia uchaguzi kwa haki na uhuru ili kupata viongozi watakaokidhi vigezo.
Pia, Jasmini Liwowa na Idrisa Asali, wasimamizi wa ngazi ya vijiji, wamesisitiza kuwa mafunzo hayo yatasaidia katika hatua zote za uchaguzi, kuanzia kwenye kujiandikisha kwa wapiga kura hadi kwenye zoezi zima la uchaguzi.
Mafunzo haya ni muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi na kwa kufuata sheria.