Viongozi vyama vya siasa wapata maelekezo uchaguzi serikali za mitaa
30 September 2024, 08:08 am
Huu ni uchaguzi unaowaweka madarakani viongozi wa mitaa, vijiji, vitongoji na wajumbe wake ambapo kanuni za mwaka huu zinamtaka mgombea katika nafasi mbalimbali kuwa na umri zaidi ya miaka 21 na mwenye sifa ya kuchagua ni yule mwenye umri kuanzia miaka 18
Na Musa Mtepa
Viongozi wa vyama vya siasa halmashauri ya Mtwara vijijini September 29, 2024 wamepewa maelekezo ya kanuni juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27,2024 kote nchini.
Wakizungumzia maelekezo hayo viongozi hao wameonesha kufurahia kitendo cha serikali kutoa maelekezo kabla ya kuanza kwa michakato ya uchaguzi kuanza huku wakiahidi Kwenda kutoa elimu kwa wanachama wao.
Aidha kwa upande wa Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Mtwara vijijini Ndug, Abeid Abeid Kafunda amewataka viongozi hao Kwenda kutoa elimu juu ya kanuni za uchaguzi ili kuepuka sintofahamu zinazoweza kujitokeza .
Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika November 27,2024 kote nchini ikiwa katika nafasi za wenyeviti wa mitaa,vijiji,vitongoji na wajumbe wake.