Jamii FM

Waziri Bashe kuzindua kiwanda cha kubangua korosho Mtwara

30 September 2024, 01:13 am

Mrajisi wa vyama vya ushirika Dkt. Benson Ndiege akizungmza na Waandishi wa habari kuelekea katika uzinduzi wa kiwanda cha kubangua Korosho mkoani Mtwara(picha na Musa Mtepa)

Suala la viwanda kumilikiwa na wakulima ni jambo la umuhimu na wakulima hawawezi kumiliki viwanda hivyo pasipo kushirikiana na vyama vya ushirika pamoja na usimamizi wa tume ya ushirika nchini.

Na Musa Mtepa

Waziri wa Kilimo Husein Bashe, tarehe 1 Oktoba 2024 anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kiwanda cha kubangua korosho kinachomilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Tandahimba na Newala (TANECU) Ltd, kilichopo kijiji cha Mmovo, wilaya ya Newala, mkoani Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Benson Ndiege, amesema kiwanda hiki ni cha kwanza  nchini kitakachomilikiwa na chama cha ushirika.

Sauti ya 1 Dkt Benson Ndiege Mrajis wa vyama vya ushirika nchini.
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyotolewa na Mrajis wa vyama vya ushirika Dkt Benson Ndiege juu ya uzinduzi wa kiwanda cha kubangulia korosho cha TANECU (picha na Musa Mtepa)

Dkt Ndiege ameeleza kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kubangua tani 3,500 za korosho kwa mwaka, zenye thamani ya shilingi bilioni 3.4.

Sauti ya 2 Dkt Benson Ndiege Mrajisi wa vyama vya ushirika Nchini.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Ndug. Frances Alfred, amekipongeza chama kikuu cha TANECU kwa ujenzi wa kiwando hicho huku akieelezea mwenendo wa soko la korosho ulimwenguni kwa miaka mitano ijayo ni katika korosho karanga kunako tokana na hitaji wa watumiaji na walaji wa zao hilo.

Sauti ya Frances Alfred Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania
Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Korosho Tanzania Ndug. Frances Alfred akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Malengo ya vyama vya ushirika katika Mkoa wa Mtwara ni kujenga zaidi ya viwanda 20 vya kubangua korosho, ili kuongeza thamani ya zao hilo .