Jamii FM
Jamii FM
30 June 2025, 17:11 pm

Hii ni ziara ya kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania katika mkoa wa Mtwara ambapo alifanya mazungumzo na mkuu wa mkoa na kutembelea Bandari ya Mtwara na kujionea inavyofanya kazi
Na Musa Mtepa
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, leo June 30, 2025 ametembelea mkoa wa Mtwara na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Patrick Sawala, pamoja na kutembelea Bandari ya Mtwara katika ziara ya kidiplomasia.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kanali Sawala amesema ujio wa Balozi Lentz unaangazia masuala ya diplomasia ya kiuchumi na fursa za uwekezaji mkoani Mtwara.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Mtwara, Bw. Ferdinand Nyathi, amesema kuwa ziara hiyo inalenga kubaini maeneo ya ushirikiano baina ya Marekani na Tanzania, hususan katika kuimarisha huduma za bandari.

Aidha, Bw. Nyathi ameongeza kuwa ziara hiyo ni ishara njema kwa diplomasia ya uchumi kati ya mataifa haya mawili.

Ziara hii ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Marekani na Tanzania, hasa katika maeneo ya kimkakati kama bandari, biashara na uwekezaji.