Wadau waombwa kuwekeza sekta ya utalii Mtwara
30 June 2024, 14:21 pm
Wizara inaunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi ya Trade Aid katika kutangaza,kutunza na kuhifadhi mji Mkongwe wa Mikindani ambao kwa mujibu kisheria mji huo umetangazwa kuwa mji wa hifadhi.
Na Musa Mtepa
Watanzania na wadau wa maendeleo wameombwa kuwekeza katika mkoa wa Mtwara kutokana na kuwepo kwa fursa mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuwa na Mazingira rafiki,vivutio vizuri vya utalii Pamoja na kutamalaki kwa hali ya amani na usalama.
Wito huo umetolewa Juni 29,2024 na mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mikindani(Mikindani day) yaliyofanyika katika viwanja vya mji Mkongwe wa Mikindani ambapo amesema kuwa watu wote wenye mapenzi mema ndani na nje ya Tanzania kufika na kuwekeza Mtwara katika Nyanja mbalimbali kama vile katika sekta ya utalii.
Aidha mkuu wa mkoa amesema kuwa katika mkoa wa Mtwara umekuwa na vivutio vizuri vya utalii vinavyoweza kuleta watu kujionea na kuwekeza huku akivitaja kuwa utaduni wa uchongaji wa vinyago kwa kabila la Wamakonde,Shimo la mungu lilopo Newala na uwepo wa kaburi linalodhaniwa kuzikwa mtu mrefu kuwahi kutokea mkoani Mtwara lilopo mtaa wa Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Kwa upande wake katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) Filbert Bayi kama Mwanariadha wa kimataifa ameiomba Wizara inayohusika na mambo ya kale na utalii kuelekeza nguvu zake kutangaza utalii uliopo Mikindani.
Akimwakilisha katibu mkuu na mkurugenzi wa Idara ya mambo ya kale Christognas Ngivingivi muhifadhi mkuu wa malikale kutoka idara ya mambo ya kale iliyopo chini ya wizara ya maliasili na utalii makao makuu Dodoma amesema kwa mujibu wa sheria na Sera ya mali kale wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali kwa kazi kubwa zinazofanywa katika kutangaza na kutunza mali kale hizo.
Maadhimisho ya Siku ya Mikindani (Mikindani day) kwa mwaka huu yamezinduliwa tarehe 23,6,2024 ambapo kumeshuhudiwa matukio mbalimbali ya kitalii yakifanyika ambapo mapema juni 29,2024 kumefanyika Mikindani Marathoni,Mashindano ya Ngoma za asili,Mashindano ya kuogelea,mashindano ya kusukuma Mitumbwi na mengineyo dhamira kuu ikiwa katika kutangaza vivutio vya utalii kupitia michezo hiyo