Kafunda ataka uelewa kanuni za uchaguzi Mtwara Vijijini
29 September 2024, 00:35 am
Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa serikali imejikita katika kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wote wenye sifa wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ili waweze kushiriki katika kuchagua kiongozi wanae mtaka
Na Musa Mtepa
Msimamizi wa uchaguzi katika Halmashauri ya Mtwara Vijijini, Abeid Abeid Kafunda, amezungumza na makundi mbalimbali kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024. Katika mazungumzo yake, Kafunda amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kanuni na sifa zinazohitajika kwa wagombea na wapiga kura.
Kafunda amewakumbusha wajibu wa makundi hayo kuwa na utaratibu katika shughuli zao na kuendelea kuelimisha vijana na jamii kuhusu taratibu za uchaguzi.
Viongozi wa dini na wazee kutoka kijiji cha Msangamkuu wameeleza kuridhishwa na juhudi za serikali katika kuwajengea uelewa huku wakiahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uchaguzi.
Makundi yaliyoshiriki ni pamoja na vijana, watu wenye ulemavu, viongozi wa dini, wazee wa kimila, na asasi za kiraia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufikisha elimu kwa jamii nzima.