TGNP kuhamasisha wanawake, vijana kushiriki nafasi za uongozi Mtwara
28 June 2024, 16:00 pm
Na Musa Mtepa
Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP umeendelea na zoezi la kutoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Mkunwa juu ya Mila na tamaduni zinazo sababisha Wanawake kutoshiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi na maamuzi katika jamii.
Wakizungumza baada ya mafunzo ya siku moja yaliyofanyika Juni 27,2024 katika shule ya Msingi Mkunwa Wananchi hao wamesema kupitia TGNP wamekuwa wakipata Elimu ya ukatili wa kijinsia,mila kandamizi Pamoja na uongozi ambayo kwa namna moja au nyingine imeanza kuleta matokeo Chanya kwa jamii nyingi katika kata hiyo.
Salumu Ali Alawi mkazi wa Kijiji cha Mkunwa amesema kupitia mafunzo hayo wamepata maarifa ya Kwenda kuhamasisha jamii katika kuondoka na tamaduni hasi wanazofundishwa Watoto wakiwa katika sherehe ya jando na unyago.
Sauti ya 1 Salumu Ali mkazi wa Kijiji cha Mkunwa
Naye Hamidu Lipea na Fadhila Selemani wakazi wa kata ya Mkunwa wamesema wao kama vijana kupitia mafunzo hayo wamejifunza kuwa vijana wananafasi kubwa ya kuwa viongozi katika jamii huku waki ahidi Kwenda kutoa elimu kwa vijana wengine juu ya ushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.
Sauti ya 2 Hamidu Lipea na Fadhila Selemani vijana na wakazi wa kata ya Mkunwa
Kwa upande wake Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia na uchumi Rebecca Mjema Kisehna kutoka mtandao wa jinsi Tanzania (TGNP) amesema kuwa Lengo kuu ya mafunzo hayo ni katika kuhimiza ushiriki wa wanawake na vijana katika nafasi mbalimbali za siasa na uongozi .
Pamoja na hayo Rebecca Mjema amesema kuwa changamoto kubwa aliyoigundua katika jamii nyingi ni za Tanzania ni kuwepo kwa mila ya Jando na Unyago ambapo amegundua kuwa mafunzo yanayotolewa wakati wa jando na unyago kutoendana na umri wa mtoto.
Sauti ya Rebecca Mjema Mwanaharakati wa Masuala ya kijinsia na uchumi kutoka TGNP