Changamoto za usafirishaji ,wakulima kuuza korosho kg1,kwa Tsh 2700 Mtwara
24 October 2024, 17:30 pm
Soko la awali serikali imeridhia kwasababu ya kuongeza ubanguaji wa ndani wa zao hilo hivyo chama kikuu hakiwezi kukataza mkulima kuuza mazao yao kupitia soko hilo ispokuwa wakulima wanatakiwa kuridhia wenyewe.
Na Musa Mtepa
Wakizungumza leo October 24, 2024 ,kwenye mkutano ulioitishwa na viongozi wa chama cha ushirika Namayanga (NAMAYANGA AMCOS) wakulima hao wamesema kuwa kutokana na mwenendo wa soko ulivyo na hali ya usafirishaji wake kutoka AMCOS kwenda Ghala kuu kuwa mgumu kumewasukuma kufanya maamuzi hayo.
Seifu Abdala Mnegelea Mwenyekiti wa AMCOS Namayanga amesema kilicho msuku Kuwahamasisha wakulima wa kata hiyo kuuza korosho kupitia soko la awali ni changamoto anazokutana nazo katika kusafirisha mzigo kuutoa kwenye AMCOS kupeleka kwenye Ghala kuu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi, Mtwara na Nanyumbu (MAMCU)Ltd Al-hajji Azam Mfaume maarufu Jula Jula amekiri kuwepo kwa changamoto za usafirishaji wa mizigo kutoka kwenye Maghala ya AMCOS Kwenda Ghala kuu kunako tokana na kuzidiwa kwa wasafirishaji.
Aidha Al-hajji Azam amesema wao kama chama kikuu cha ushirika hawawezi kumzuia mkulima kuuza korosha zao kupitia soko la awali kwani lipo kisheria na linatambuliwa na serikali huku akiwaomba wakulima kukubaliana na mabadiliko yaliyofanyika yenye lengo la mkusaidia mkulima Mwenyewe.