Baraza la madiwani Mtwara labatilisha umiliki wa kiwanja cha Mbunge
24 May 2024, 23:15 pm
Waheshimiwa Madiwani wameunga mkono kubatirishwa kwa kiwanja kinachosadikiwa kumilikiwa na Mbunge wa Mtwara Mjini huku mstahiki Meya akiwaagiza watendaji kuyatambua na kuyawekea alama maeneo yote yaliyopo chini ya halmashauri ili kurahisiasha utambuzi inapotokea mtu kuvamia maeneo hayo
Na Musa Mtepa
Baraza la madiwa Manispaa ya Mtwara Mikindani limebatilisha uhalali wa umiliki wa kiwanja katika eneo la Shangani mashariki kinachosadikika kumilikiwa na Mbunge wa Mtwara Mjini baada ya kamati ya kudumu ya mipango miji,Ardhi na ujenzi kujiridhisha kuwa eneo hilo kuwa ni mali ya halmashauri.
Akitoa maagizo kwa Mkurugenzi mtendaji na watendaji wa halmashauri kupitia baraza la madiwa lililofanyika leo tarehe 24/5/2024 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mh. Shadida Ndile amesema kuwa maeneo yote ya halmashauri yatambulike na kuwekewa alama zinazojulikana ili kama kuna mtu anataka kuchukua eneo kinyume na taratibu aweze kutambulika
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya mipango miji,ardhi na ujenzi ya manispaa ya Mtwara Mikindani ambae pia ni Diwani wa kata ya Naliendele Mh. Masudi Dali amesema baada ya kupitia katika vikao vya kamati juu ya uhalali na historia waligundua kuwa mmiliki wa eneo hilo hajafuata utaratibu wa umiliki na kuliomba baraza kubatilisha umiliki wake.
Naye Diwani wa kata ya Vigaeni Manispaa ya Mtwara Mikindani Mh Saidi Ali Nassoro(White) amesema kuwa halmashuri ya Manispaa ya Mtwara mikindani lilipima eneo la Shangani kuanzia mwaka 1985 na eneo hilo liliachwa kwa ajili ya matumizi ya serikali na sio mtu binafsi.
Abuu Mohamedi Abdala ni Diwani wa kata ya Shangani ambae pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya mipango miji, ardhi na ujenzi amesema kuwa baraza imetoa maamuzi ya kukifutia hati kiwanja hicho kwasababu ya taratibu za kawaida hazikufuatwa ikiwemo mwombaji kuomba kumilikishwa na halmashauri kwakuwa lilikuwa linamilikiwa na mjomba wake .