Jamii FM

Upepo wa ajabu waezua paa la nyumba Mtwara

22 July 2024, 09:10 am

mwonekano wa paa la Nyumba liloezuliwa na upepo(Picha na Musa Musa)

Limeanzia kati kati ya Bahari ,tumeona taswira muonekano kama Samaki wawili wakubwa wenye mvuke wa moshi na upepo mkubwa ambao umeleta taharuki ambao ulikuja kuishia kwenye nyumba ya Bwana Fadhili Ismail

Na Musa Mtepa

Watu wawili wamenusurika kujeruhiwa na paa la nyumba baada ya kutokea upepo mkali unaodaiwa kuwa ni wa ajabu katika kijiji cha Naumbu Kaskazini mkoani Mtwara.

Akizungumzia tukio hilo  Lukia Muanya Seifu manusura wa tukio hilo amesema  limetokea Julai 17, 2024 ambapo waliona taswira kama ya  Samaki wakubwa baharini ulioambatana na upepo mkali  na moshi ulioleta taharuki kwa wananchi Pamoja na kuezua paa la nyumba.

Sauti ya Lukia Muanya Seif mmiliki wa nyumba na manusura wa tukio la kuangukiwa na paa la Nyumba

Fadhili Ismaili Mume wa Lukia Muanya amesema athari kubwa iliyojitokeza kutokana na upepo huo  kuezuliwa kwa paa la nyumba ,kuharibiwa kwa chombo cha kuvulia Samaki Baharini(Mtumbwi) na pamoja na kubomolewa kwa Choo huku akiomba msaada wadau kumsaidia ili makazi yake yarejee kama zamani.

Sauti ya Fadhili Ismail mume wa Lukia Muanya
Nyumba iliyoezuliwa na upepo wa ajabu(Picha na Musa Mtepa )

Aidha kwa upande wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema tukio hilo hawajawahi kuliona tangu kuzaliwa kwao huku wakiwa na hofu kwa kuhofia huenda kikajirudi tena katika Kijiji hicho.

Sauti ya Wananchi wa Naumbu kaskazini

Wakizungumzia hatua zilizochukuliwa katika kumsaidia Lukia Muanya na Bw Fadhili Ismaili Mwenyekiti wa kitongoji na Kijiji cha Naumbu kaskazini wamesema wao kama uongozi wa Kijiji wapo kwenye mchango wa fedha wa kuisadia familia hiyo ili waweze kurejea katika hali yake awali.

Sauti ya mwenye kiti wa kitongoji na mwenyekiti wa Kijiji cha Naumbu