TARI kushirikisha wakulima kwenye utafiti wa mbegu
22 June 2024, 20:21 pm
Katika siku zijazo tunataka mkulima wa korosho awe na misimu miwili ana ule msimu wa korosho karanga na msimu wa bibo kwani siku hizi bibo linaonekana ni kitu cha kutupwa kumbe kuna bidhaa ambazo zinapatikana kama mvinyo (wine),Ethanol inayotokana na bibo pamoja na juisi ya bibo hivyo tunahakikisha kuwa tunapata bidhaa zote katika ngazi ya kibiashara.
Na Grace Hamisi
Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI),Dkt. Thomas Bwana amefanya ziara ya siku mbili katika kituo cha utafiti wa kilimo (TARI) Naliendele na kutembelea sehemu za uzalishaji wa miche ya mikorosho na michikichi pamoja na kiwanda cha kubangua korosho kilichopo kituoni hapo.
Akiwa katika ziara hiyo Dkt Thomas amesema kuwa kwa sasa watahakikisha wanawashirikisha wakulima katika utafiti wa uzalishaji wa mbegu ili kusaidia na wao kujitengenezea mbegu iliyobora zaidi .
Aidha Dkt Thomas meongeza kuwa (TARI) Naliendele imefanya vizuri kwenye utafiti wa korosho kwa upande wa magonjwa ya ubwiri unga huku aina nane (8) za mbegu za korosho zilizofanyiwa utafiti na kubainika kuwa na uhimilivu mkubwa wa magonjwa.
Hata hivyo Dkt Thomas Bwana amesema kwa sasa wanataka kuwapa wakulima fursa ya kujaribu mazao tofauti na waliyoyazoea kama migomba na michikichi kutokana na mimea hiyo kuwa na uhitaji mkubwa katika uazalishaji wa mafuta ambayo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa katika uzalishaji wa mafuta ili kuachana na uagizaji kutoka nje ya nchi.
Sauti ya 3Dkt Thomas Bwana mkurugenzi mkuu wa TARI