Jamii FM

Meli iliyobeba makasha 459 yatia nanga bandari ya Mtwara

20 September 2024, 19:24 pm

Meli iliyobeba makasha (Containers) 459 ikiwa imetia nanga katika Bandari ya Mtwara (Picha na RS Mtwara)

Msimu wa  2023/2025 meli za kusafirsha korosho zilichelwa kufika ktika bandari ya Mtwara hali iliyoleta changamoto kwa wanunuzi wa zao hilo ambapo kwa mwaka huu imekuwa tofauti meli na makasha yamefika mapema kabla hata ya mnada wa kwanza wa zao hilo.

Na Musa Mtepa

 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bi Zainab Telack, amewahakikishia wanunuzi wa korosho kuwa serikali ipo tayari kuhakikisha vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya usafirishaji wa korosho kupitia bandari ya Mtwara vinapatikana na vipo tayari.

Sauti ya Bi Zainab Telack Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack akizungumza na waandishi wa habari baada ya ujio wa meli hiyo

Bi Telack ameyasema hayo wakati wa mapokezi ya meli ya MV GH TRAMONTANE, iliyobeba makasha zaidi ya 450, ambayo imewasili bandari ya Mtwara ikiwa katika maandalizi ya msimu mpya wa korosho wa 2024/2025.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) mkoa wa Mtwara, Bw. Ferdinand Nyati, amesema ujio wa meli hiyo ni kiashiria cha kufungua msimu mpya wa usafirishaji wa korosho. Ameongeza kuwa katika msimu wa 2023/2024, meli zilifika mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Sauti ya Ferdinand Nyati Meneja wa TPA Mtwara
Meneja wa TPA Mtwara Ferdinand Nyati

 Kwa niaba ya mawakala wa meli, Mwakilishi wa kampuni ya usafirishaji ya IPL, Bw. Rajeiv Grovery, ameishukuru serikali kwa mazingira mazuri ya usafirishaji na kuahidi kuendelea kutumia bandari ya Mtwara katika usafirishaji wa korosho kama ilivyokuwa mwaka uliopita.

Sauti ya Bw Rajeiv Grovery Mwakilishi wa kampuni ya PIL

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Mwalimu Saidi Nyengedi, ameipongeza mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini kwa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM.

Sauti ya Mwalimu Saidi Nyengedi Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara