Makala – Elimu ya Usalama Barabarani kwa Watu Wenye Ulemavu
20 June 2024, 16:00 pm
Watu wenye ulemavu wanasisitiza umuhimu kwa watumiaji wa barabara kuwapa kipaumbele kutokana na changamoto wanazokutana nazo wanapotumia barabara. Kila mmoja wetu ana jukumu la kuhakikisha usalama barabarani, si jukumu la serikali pekee.
Abeid Yusufu Lukanga, ambaye ni mlemavu anayetumia baiskeli, ameeleza kuwa alama zinazowatambulisha watu wenye ulemavu zipo lakini baadhi ya madereva wanashindwa kuzitambua. Hii ni hatari kwa usalama wao wanapokuwa barabarani.
Mkaguzi msaidizi wa jeshi la Polisi Rebeca Milele kutoka ofisi ya usalama barabarani mkoa wa Mtwara amethibitisha kwamba wanatoa elimu ya usalama barabarani kupitia shule na vyombo vya habari ili kuhakikisha kuwa kila mtu, ikiwemo watu wenye ulemavu, wanafikiwa na elimu hiyo.
Tushirikiane kupunguza ajali za barabarani na kuokoa maisha ya watu wenye ulemavu. Kusikiliza makala hii kutakusaidia kuelewa zaidi.