Jamii FM
Jamii FM
19 December 2025, 11:29 am

Na Musa Mtepa
Makala haya yanaelezea jukumu la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika kutoa taarifa na utabiri wa hali ya hewa kwa lengo la kulinda usalama wa maisha, mali na shughuli za kiuchumi, hususan sekta ya kilimo ambayo ni tegemeo la Watanzania wengi.
Kupitia mazungumzo na wataalamu wa hali ya hewa kutoka TMA Kanda ya Kusini na Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI–Naliendele, makala yanafafanua hali ya msimu wa mvua wa mwaka 2025/2026 unaotarajiwa kuwa wa wastani hadi chini ya wastani, hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Aidha, makala yanaangazia tahadhari na ushauri unaotolewa kwa wakulima, ikiwemo matumizi ya mazao yanayostahimili ukame na mbinu bora za kilimo, pamoja na mikakati ya wakulima wa mikoa ya kusini katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa mvua.
Kupitia ushuhuda wa wakulima, makala yanabainisha umuhimu wa kuzingatia utabiri wa hali ya hewa ili kupunguza hasara, kulinda usalama wa chakula na kuongeza ustahimilivu wa uzalishaji wa kilimo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.