Jamii FM

Elimu ya dini suluhisho la uvunjifu wa maadili nchini

19 September 2024, 12:52 pm

Viongozi wa Dini, Vijana na Jeshi la polisi wakiwa studio namba mbili ya Jamii FM Radio katika mahojiano ya nini kifanyike ili kuondoa matukio ya uvunjifu wa maadili na ukatili nchini

Ukatili na uvunjifu wa maadili katika jamii umesababishwa na mambo mbalimbali kama vile wazazi kutosimama katika nafasi zao kwa Watoto, ukuaji wa teknolojia na kutofuata misingi ya dini hali inayopelekea kila kukicha kutokea matukio ya kikatili na uvunjifu wa maadili.

Na Musa Mtepa

Katika juhudi za kupambana na vitendo vya ukatili na uvunjifu wa maadili yanayoendelea kujitokeza nchini, jamii imetakiwa kuwekeza zaidi katika elimu ya dini.

Hayo yamesemwa Septemba 18, 2024, na viongozi wa dini, wanasiasa, na vijana katika mahojiano maalumu na Jamii fm redio kuhusu hatua za kuchukua ili kutokomeza vitendo hivyo.

Salumu Musa Mkonga, katibu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Mtwara mjini, amesema kuwa vitendo hivyo vinatokana na kukosekana kwa elimu ya dini katika jamii, hali inayosababisha watu kukosa hofu ya Mungu.

Sauti ya Salumu Musa Mkonga katibu wa baraza la waislamu (BAKWATA) Mtwara mjini

Kwa upande wake, Ezekiel Shikombe ambaye ni mchungaji wa Kanisa la African Church Tanzania mkoa wa Mtwara, amesisitiza kuwa maadili yanapaswa kuanzia katika ngazi ya familia.

Sauti ya Ezekiel Shikombe mchungaji wa kanaisa la African Church Tanzania

Akijibu swali kuhusu njia bora za kujenga jamii yenye hofu ya Mungu, Iddi Mangongo, mwakilishi wa vijana kutoka kata ya Chuno, ameeleza umuhimu wa wazazi na walezi kuwa na uataratibu wa kuandaa watoto katika misingi ya maadili mema.

Sauti ya Iddi Mangongo kijana kutoka kata ya chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani

Wito huu unakuja wakati ambapo jamii inakabiliwa na changamoto nyingi zinazohitaji umoja na uelewa mzuri.

Kila kiongozi amehimiza umuhimu wa kushirikiana ili kufanikisha lengo la kujenga jamii iliyo na maadili na hofu ya Mungu, hivyo kupunguza vitendo vya ukatili na uvunjifu wa maadili nchini.