Jamii FM
Jamii FM
19 June 2025, 18:53 pm

“Mabadiliko makubwa yameanza kujitokeza ambapo wanawake wameanza kushika nafasi muhimu za uongozi katika nyanja mbalimbali kama siasa, uchumi na hata uongozi katika taasisi za dini.”
Na Mwanahamisi Chikambu
Katika historia ya jamii nyingi duniani, mwanamke ameonekana kuwa nyuma katika masuala ya uongozi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo mila na desturi pamoja na mtazamo hasi kutoka kwa jamii. Hata hivyo, katika karne ya 21, mabadiliko makubwa yameanza kujitokeza ambapo wanawake wameanza kushika nafasi muhimu za uongozi katika nyanja mbalimbali kama siasa, uchumi, na hata uongozi katika taasisi za dini.
Pamoja na jitihada za serikali na mashirika mbalimbali, familia kama taasisi ya msingi katika jamii ina nafasi ya kipekee ya kuhakikisha mwanamke anakuwa kiongozi bora. Katika makala hii, tumewazungumza watoto wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkangala Kusini, Mwenyekiti wa Kata ya Mihambwe, baadhi ya wananchi, pamoja na Mwenyekiti wa Mkangala Kusini, Kata ya Naliendele, ili kufahamu mchango wa familia katika kukuza viongozi wanawake.
Kusikiliza makala haya Bonyeza hapa