Jamii yatakiwa kufahamu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji
18 April 2024, 21:57 pm
Shughuli zinazofanywa karibu na vyanzo vya maji zimekuwa zikihatarisha uwepo wake huku mamlaka zikiombwa kuendelea kutoa elimu ya athari hasi na umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji.
Na Msafiri Kipila
Mammlaka zinazo simamia vyanzo vya maji zimeombwa kutoa Elimu kwa wananchi juu ya athari hasi na umuhimu wa utunzaji wake ili kuepuka kuharibiwa kunakotokana na ongezeko la mahitaji na iadadi ya Watu.
Wakizungumza na Jamii fm radio 16/4/2024 baadhi ya Wananchi wa kata ya Mtawanya Manispaa ya Mtawara Mikindani wamesema kuwa ili kuepuka uharibifu wa vyanzo vya maji mamlaka na idara husika wanatakiwa kushirikiana na serikali za mitaa ili kurahisha kufikisha elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji kwa njia rahisi.
Sharifu Kassimu Namkanda mkazi wa mtaa wa Mtawanya Manispaa ya Mtwara Mikindani amesema vyanzo vya vilivyopo ni vya muda mrefu hivyo uhitaji wake ni mkubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo watu walikuwa wachache.
Akizungumzia Uelewa wa Wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji mkuu wa kitengo cha uhamasishaji kutoka ofisi ya bodi ya maji bonde la Ruvuma na pwani ya kusini Bw Dicksoni Maganga amesema kuna baadhi ya wananchi wanaamini kuwa maji ni rasilimali ambayo inayotoka kwa Mungu hali inayowafanya kutowajibika katika utunzaji wa vyanzo hivyo.
Aidha naye Bonifasi Msemwa mkuu wa kitengo cha utunzaji bonde kutoka ofisi ya bodi ya maji bonde la ruvuma na pwani ya kusini ameitaka jamii kuhakikisha inatunza vyanzo vya maji kwa kutofanya shughuli yeyote hatarishi katika eneo la chanzo .