Jamii FM

Msangamkuu Beach Festival kuzinduliwa rasmi 27 Disemba 2024 Mtwara

17 December 2024, 18:25 pm

Huu ni mwaka wa  nne wa tamasha la Msangamkuu Beach Festival ambapo miaka yote huadhimishwa mwezi Disemba ya kila mwaka na  lengo likiwa kutangaza vivutio vya utalii katika mkoa wa Mtwara

Na Musa Mtepa

Tamasha la Msangamkuu Beach Festival, linalohamasisha utalii katika mkoa wa Mtwara na kusini kwa ujumla, linatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 27 Disemba 2024 katika fukwe za Msangamkuu. Tamasha hili litapambwa na burudani mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, akizungumzia tamasha hilo, amewaalika wananchi wa ndani na nje ya mkoa wa Mtwara kushiriki, akieleza kuwa kutakuwa na matukio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ya mila na desturi za wakazi wa Mtwara pamoja na matukio mengine.

Sauti ya 1 – Kanali Patrick Sawala, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara

Aidha, Kanali Sawala amesema kuwa dhamira kuu ya tamasha hili ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mkoa wa Mtwara na kukuza fursa za uwekezaji, hasa katika fukwe zilizopo mkoani humo.

Sauti ya 2 – Kanali Patrick Sawala, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Naye, Emmanuel Mwambe, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, amewaomba wananchi kujumuika kwa pamoja kwani kumeandaliwa siku maalum kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na familia kwa ujumla.

Sauti ya Emmanuel Mwambe, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Msangamkuu Festival.

Brayton Kawiche, Afisa Muhifadhi wa Mji Mkongwe wa Mikindani, amesema tamasha la Msangamkuu linachangia sana kwa mkoa na kwa mtu mmoja mmoja, kwani limekuwa likiwakutanisha watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara, wasanii, na wanamichezo, hali inayochochea kukuza uchumi na utalii wa Mtwara.

Sauti ya Brayton Kawiche, Afisa Muhifadhi Mji Mkongwe wa Mikindani.