Lindi mwambao wauza korosho tani 1,896 mnada wa sita
16 November 2024, 23:39 pm
Mnada huo ambao umeendeshwa kwa njia ya mtandao kwa usimamizi wa soko la bidhaa Tanzania TMX, umefanya korosho zilizouzwa nchini matika msimu huu wa 2024/2025 kufikia Tani 310,000.
Na Mwandishi wetu
Chama Kikuu cha Ushirika LINDI MWAMBAO kimeumza jumla ya Tani 1,896 za Korosho kwa bei ya Shilingi 2,900/= katika mnada wa sita uliofanyika Kijiji cha Nyengedi Wilaya ya Lindi leo tarehe 16 Novemba 2024.
Mnada huo ambao umeendeshwa kwa njia ya mtandao kwa usimamizi wa soko la bidhaa Tanzania TMX, umefanya korosho zilizouzwa nchini katika msimu huu wa 2024/2025 kufikia Tani 310,000.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima, Mjumbe wa bodi ya Lindi Mwambao Said Mwinyi, amewataka wakulima kuendelea kuvuna Korosho zao na kuzihifadhi kulingana na maelekezo yanayotolewa na wataalm wa ubora.
“Kama mnavyoona dalili za mvua zimeshaanza, hivyo tujipange kwa siku zijazo kwenye eneo la uhifadhi wa Korosho zetu ili zibakie kwenye ubora unaostahili”
Kwa upande wake Afisa Biashara wa Soko la Bidhaa Tanzania TMX Bw. Mahama Kadikilo, ameeleza mwenendo wa minada kwa mkoa wa Lindi unaendelea vizuri na wananchi wanazidi kuelewa faida za kufanya mauzo kwa njia ya mtandao.
“Wananchi wanashuhudia kila kitu kupitia mfumo huu, ndio maama unawaona wakishiriki kila hatua mwanzo mpaka mwisho wa mnada na hatimae wanafanya maamuzi ya kuuza korzao” amesema Mahama wakati akihojiwa na waandishi wa habari baada ya mnada.