Jamii FM
Jamii FM
16 May 2025, 11:19 am

Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kutoka kituo cha Naliendele na vituo vingine nchini wametakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma katika kutekeleza majukumu yao
Na Mwanahamisi Chikambu
Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kutoka kituo cha Naliendele na vituo vingine nchini wametakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Bi. Judith Nguli, mnamo Mei 13, 2025, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya maadili kwa watumishi wa umma, yaliyofanyika katika kituo cha TARI Naliendele, mkoani Mtwara.
Bi. Nguli amesisitiza kuwa maadili ni msingi wa utendaji bora wa kazi, na amewahimiza wataalamu wa kilimo kutumia ujuzi wao kukuza mazao ya chakula kama mpunga, mbogamboga na mahindi ili kuinua kipato na ustawi wa wakulima nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo cha TARI Naliendele, Bi. Geradina Mzena, amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea watumishi misingi imara ya maadili ambayo yatasaidia katika kufanya tafiti zenye tija na kutatua changamoto mbalimbali za wakulima.
Washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kuwa yamekuwa ya manufaa makubwa kwao, kwani yamewakumbusha umuhimu wa kuwa waadilifu, kuwajibika, na kutoa huduma bora kwa wakulima na jamii kwa ujumla.
