Jamii FM

RC Sawala aongoza matembezi kuhamasisha uandikishaji serikali za mitaa

14 October 2024, 13:51 pm

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala akiongoza matembezi ya kuhamasisha ujiandikishaji kwenye orodha la wapiga kura (Picha na Musa Mtepa)

Matembezi haya yenye lengo la kuhamasisha ushiriki kila mmoja mwenye sifa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa November 27,2024 kote nchini ambapo kwa hatua ya awali uandikishaji wa orodha ya wapiga kura tayari umeshaanza October 11, 2024.

Na Musa Mtepa

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, ameshiriki matembezi na mazoezi ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

 Katika tukio hilo, amewahimiza wananchi kutumia muda uliobaki kujiandikisha ili waweze kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya maendeleo yao.

Sauti ya 1 Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara.
Kanali Sawala akiwa kwenye mazoezi ya kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa (Picha na Musa Mtepa)

Kanali Sawala pia amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani na kuwataka wananchi wasikubali kutumiwa na watu au makundi yoyote kuhamasisha vurugu katika kipindi cha uchaguzi.

Sauti ya 2 Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mtwara Mjini, Salumu Naida, ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kujiandikisha mapema badala ya kusubiri hadi siku za mwisho kujitokeza kwa wingi kama uzoefu unavyoonesha kwa baadhi ya matukio ya nyuma.

Sauti ya Saidi Nnaida Mwenyekiti wa CCM Mtwara Mjini.

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria matembezi hayo wameonyesha furaha na kuahidi   kulinda amani katika mkoa wa Mtwara kuelekea uchaguzi serikali za mitaa.

Sauti ya Wananchi waliojitokeza kwenye matembezi ya kuhamasisha ushiriki wa wananchi uchaguzi wa serikali za mitaa November 27,2024.
Maafisa usafirishaji wakishiriki matembezi ya kuhamasisha undikishaji wa orodha ya wapiga kura na uchaguzi wa serikali za mitaa (Picha na Musa Mtepa)