Wavuvi waliopotea baharini Mtwara bado hawajaonekana
14 May 2024, 08:06 am
Boti hiyo ambayo ilikwenda baharini jioni ya tarehe 9/5/2024 kwa matarajio ya kurudi asubuhi ya tarehe 10/5/2024 lakini hawakufanikiwa kurudi baada ya kupata hitilafu na walinipigia simu kuanzia saa kumi na moja hadi saa sita mchana wakaniambia mwenyekiti simu zetu zinaisha chaji kuanzia hapo hatukuwapata tena
Na Musa Mtepa
Boti ya uvuvi iliyobeba Wavuvi watatu wanaovua Bahari ya Hindi Mkoani Mtwara inayohofia kupotea kwa kuzama Baharini wakati wakiwa katika shughuli za uvuvi hadi kufikia leo 13/5/2024 bado haijonekana .
Akizungumza na Jamii fm radio mwenyekiti wa jumuia ya Wavuvi Manispaa ya Mtwara Mikindani Mzee Sheha Shante amesema hadi kufikia leo tarehe 13/5/2024 wavuvi hao hawajaonekana na jitihada za kuwatafuta zikiwa zinaendelea ambapo Boti tatu za watafutaji zimeshafika katika maeneo ya kilwa na Mafia katika utafutaji huo
Hata hivyo Mwenyekiti huyo ameonesha kusikitika kutokuwepo kwa wadau wa Bahari na Serikali kuwepo kwa chombo cha uokozi kitakacho Saidia kuokoa kuliko kutegemea vya taasisi nyingine ambazo zinahitaji mchakato mrefu kuvipata vyombo hivyo.
Mwenyekiti wa Soko la Feri Manispaa ya Mtwara Mikindani Mwinyi Mzaina amelishauri jeshi la zimamoto na uokoaji Pamoja na serikali kujipanga vizuri kwa upande wa Baharini kama walivyojipanga kwa upande wa nchikavu kwani anamini ya kuwa kama wangekuwa na vyombo vya uokoaji vya baharini wangefanikiwa kuwaokoa kwa wakati wavuvi hao.
Kwa upande wake jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mtwara zimeelezea hatua na jitihada zilizofanyika katika kuwaokoa wavuvi hao amabapo walifanikiwa kupata Boti ya polisi (Police Marine) kwa ajili ya kuwatafuta lakini hawakuweza Kwenda kwa wakati kutokana na changamoto ya Muda(usiku).
Wavuvi waliopotea ni Hashimu Faki,Hamisi Zahoro na Athumani Hamueji waliokuwa wanatumia Boti inayo julikana kama Marua ambao inasemekana wana asili ya visiwa vya Zanzibari.