Blandina Chilumba aahidi maendeleo zaidi baada ya ushindi wa uchaguzi
13 December 2024, 15:54 pm
Blandina Chilumba ametetea nafasi yake katika uchaguzi uliopita hii inadhihirisha kuwa wananchi wa mtaa wa Mihambwe bado wana Imani naye.
Na Mwanahamisi Chikambu
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mihambwe, Kata ya Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Blandina Chilumba, ameendelea kutetea kiti chake baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.
Bi. Chilumba ameahidi kutekeleza ahadi zake na kuendelea na kazi alizoanzisha ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa mtaa huo.
Akizungumza na Jamii FM redio, Bi. Chilumba amewaomba wananchi wa Mtaa wa Mihambwe kuendelea kutoa ushirikiano ili kushirikiana kutatua changamoto zinazowakabili na kusaidia kuendeleza ujenzi wa ofisi ya mtaa huo.
Aidha, Bi. Chilumba ameviomba vyama vya siasa kukubali matokeo ya uchaguzi na ameahidi kuhakikisha anamaliza miradi iliyozinduliwa katika mtaa huo.
Wananchi wa mtaa wa Mihambwe, Abillah Masudi na Hadija Swalehe, wamesema kuwa wameamua kumpa tena nafasi ya kuongoza kwa sababu kiongozi huyo anasikiliza na kuelewa changamoto zao.