Jamii FM

 Mtwara DC, NMB wahamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura

12 October 2024, 11:00 am

Abeid Abeid Kafunda na meneja wa kanda,vikundi na huduma za kibenki vijijini Dismasi Prosper wakishiriki Jogging(Picha na Musa Mtepa)

Lengo la jogging na michezo mingine ni katika kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji kwenye daftari la wapiga kura lilionza rasmi jana October 11, 2024 kote nchini.

Na Musa Mtepa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara DC, Abeid Abeid Kafunda, ameshiriki katika Jogging ya kuhamasisha wananchi, iliyofanyika leo tarehe 12 Oktoba 2024, kwa ushirikiano wa Benki ya NMB.

Zoezi ambalo limeandaliwa ili kuhamasisha wananchi kushiriki katika uandikishaji wa daftari la wapiga kura, ambalo lilianza tarehe 11 Oktoba 2024.

Katika hotuba yake mbele ya wananchi wa Mkunwa, Kafunda amesisitiza umuhimu wa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo, akiwataka wananchi  kushiriki kikamilifu.

Sauti ya Abeid Abeid Kafunda Mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara dc

Kwa upande mwingine, Dismas Prosper, Meneja wa Kanda wa NMB, ameelezea kuwa benki hiyo inatumia fursa ya NMB Kijiji Day kuhamasisha uandikishaji wa wapiga kura na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zao za benki.

Prosper ameongeza kuwa ni muhimu wananchi wawe na uelewa mzuri wa huduma zinazotolewa na benki hiyo ili kuweza kuzitumia vyema.

Sauti ya Dismas Prosper Meneja wa Kanda,vikundi na upelekaji wa huduma za kibenk vijijini kutoka idara ya mauzo NMB
Wananchi wakishiriki Jogging iliyofanyika katika kijiji cha Mkunwa Halmashauri ya Mtwara vijijini(Picha na Musa Mtepa)

Tukio hili linaonyesha ushirikiano mzuri kati ya serikali na sekta binafsi katika kukuza demokrasia na maendeleo ya jamii.