Kapela: Wanaume msiwabeze wanawake kwenye uongozi
12 July 2024, 09:42 am
Changamoto kubwa aliyokutana nayo Bw Mustafa Chona wakati anampambania mkewe kuwa diwani wa kata ya Njengwa ni kwa baadhi ya wanaume kumdhihaki kuwa anapoteza muda wa kumpambania mkewe na kujirudisha nyuma kimaendeleo kwa kuuza baadhi ya mali na mifugo ili kumsaidia mke wake katika harakati za uongozi.
Na Musa Mtepa
Wanaume wameshauriwa kuwaandaa watoto wa kike na kuwa mstari wa mbele katika kupigania na kuhakikisha mwanamke anakuwa kiongozi ili kuondoa dhana ya kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi katika jamii.
Wito huo umetolewa na Moza Salumu Kapela diwani wa kata ya Njengwa wakati wa mahojiano maalum na Jamii fm Radio ambapo amesema kuwa nafasi aliyonayo hivi sasa ni kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na mumewe na wakati mwingine amekuwa muhimizaji mkubwa katika kutekeleza majukumu yake hivyo ni wakati kwa wanaume wengine kuiga na kuwapa nguvu wanawake hasa wanapoonesha nia ya kuwa kiongozi.
Sauti ya 1 Moza Salumu kapela Diwani wa kata ya Njengwa Halmashauri yam ji Nanyamba Mtwara Dc
Aidha Mh Moza amesema kuwa kutokana na moyo na jitihada alizozionesha kwake wengi wanafikiri mume wake ni mfanyabiashara ila kiuhalisia ni mkulima tena ni mkulima wa hali ya chini.
Sauti ya 2 Moza Salumu kapela Diwani wa kata ya Njengwa Halmashauri yam ji Nanyamba Mtwara Dc
Kwa upande wake Mustafa Chona mume wa Moza Kapela diwani wa kata ya Njengwa amesema walikubaliana wote kwa Pamoja kupambania nafasi hiyo kwa kipindi kirefu kwa kuanzia katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama huku malengo yao makubwa yakiwa siku moja kuwa Diwani wa kata ya Njengwa ili aweze kuwatatulia Wananchi kero zilizokuwa zinawakabiri.
Pamoja na hayo Mustafa Chona ametoa wito kwa wanaume wanaoamini Mwanamke hawezi kuwa kiongozi katika jamii ambapo amesema kuwa wanawake wanaweza kuwa kiongozi na kusimamia vizuri na wakati mwingine zaidi ya mwanaume .
Kata ya Njengwa ni mara ya kwanza inakuwa na diwani mwanamke ambapo baada ya kuingia madaraka Mheshimiwa Moza Kapela amefanikisha upatikanaji wa uhakika wa huduma ya umeme,maji ,Barabara na miundombinu mbalimbali ya madarasa kwa shule za Msingi na Sekondari pamoja na Zahanati hali ambayo ilikuwa tofauti na hapo awali kwa viongozi wengine waliopita kwa kipindi cha Nyuma.