TANECU yauza korosho tani 3,857 kwa Tsh 4,120
11 October 2024, 15:50 pm
Mnada wa leo wameshindana makampuni 37 na korosho zote zilizouzwa zimenunuliwa na makampuni 10 hivyo makampuni 27 yamekosa korosho maana yake ni kwamba kunauhitaji wa korosho duniani na beii hii ni kutokana dunia ina uhitaji mkubwa wa korosho karanga na kutokana na hilo italeta hamasa kwa wakulima kuhudumia mashamba yao vizuri.
Na Grace Hamisi
Chama kikuu cha ushirika kinachohudumia Tandahimba na Newala (TANECU) kimefanikiwa kuuza tani 3,857 za korosho katika mnada wa kwanza uliofanyika leo, tarehe 11 Oktoba 2024, katika wilaya ya Newala, mkoani Mtwara. Ambapo bei ya juu kupitia Mnada huo ni Tsh. 4,120 na Tsh. 4,035 bei ya chini
Akizungumza katika ufunguzi wa mnada huo, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, amesisitiza umuhimu wa wakulima kuhakikisha wanazalisha korosho zenye ubora ili waweze kupata bei nzuri inayowaridhisha.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Fransis Alfred, ameeleza kuwa hadi jana, kampuni 45 zilikuwa zimekidhi vigezo na kupata leseni ya kununua korosho.
Bi. Rukia Silimu, mkulima kutoka kijiji cha Mwangaza, ameeleza furaha yake kuhusu bei hii, akisema kuwa hakuweza kutarajia mabadiliko mazuri ikilinganishwa na miaka iliyopita ambayo ilikuwa na changamoto nyingi.
Kwa ujumla, habari hii inaonyesha mwelekeo chanya katika soko la korosho, inatoa matumaini kwa wakulima wa zao hilo.