Jamii FM

Dkt. Biteko azitaka halmashauri kutumia fedha za gesi kubadilisha maisha ya wananchi

11 September 2024, 08:43 am

Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt Dotto Biteko akizungumza na Wananchi waliojitokeza kwenya hafla ya kukabidhi leseni ya uendelezaji eneo la ugunduzi wa Gasi Asilia la Ntorya.(Picha na RS Habari)

Halmashauri zilizopo kwenye miradi ya uchimbaji wa Gesi Asilia zihakikishe fedha za ushuru zina wanufaisha wananchi wa maeneo husika na sio kama hali ilivyo hivi sasa.

Na Musa Mtepa

Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt Dotto Biteko ameziagiza halmashauri zilizopo katika miradi ya Gesi kutumia fedha zitokanazo na ushuru wa uchimbaji wa gesi asilia ili kubadili maisha ya wananchi wa maeneo hayo badala ya kusubiri bajeti kutoka serikali kuu.

Dkt Biteko ametoa agizo hilo September 11, 2024 katika kijiji cha Nanguruwe mkoani Mtwara katika hafla ya kukabidhi leseni ya uendelezaji eneo la ugunduzi wa Gasi Asilia la Ntorya.

Sauti ya Dkt Dotto Biteko Naibu Waziri mkuu na Waziri wa nishati

Sambaba na hilo Dkt Biteko ametoa wito kwa kampuni ya ARA Petroleum na Ndovu kuwapa kipaumbele wakazi wa eneo la mradi utoaji wa ajira ili kutengeneza muunganiko wa wananchi na uchumi wa maeneo hayo. 

Sauti ya 2 Dkt Dotto Biteko naibu Waziri mkuu na Waziri wa nishati

kwa upande wao wakazi wa eneo hilo wameoneshwa kufurahia na ujio wa waziri huyo huku wakiiomba serikali kuwalipa stahiki zao kwa wakati ili kuondoa usumbufu baina yao.

Sauti ya Wananchi wa kijiji cha Nanguruwe

Mara ya mwisho kwa serikali kutoa leseni ya uendelezaji wa visima vya gesi ilikuwa mwaka 2006.