Wakulima washauriwa kuzingatia ubora wa ufuta ukiwa shambani
11 May 2024, 14:10 pm
Na Musa Mtepa
Wakulima wa ufuta wameaswa kuzingatia mambo ya msingi kabla na baada ya kuvuna ili waweze kupata soko zuri la zao hilo.
Wito huo umetolewa tarehe 10/5/2024 na mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa kilimo ( TARI) Naliendele Dr Fortunus Kapinga alipotembelewa na Wanafunzi wa chuo cha mafunzo ya kilimo Mtwara (MATI) ambapo amesema kuwa wakulima wanatakiwa kuangalia umuhimu wa ubora wa ufuta wenyewe kwa kuanzia shambani hadi kwenda kwenye soko.
Aidha Dr Kapinga amesistiza ubora pia unaweza kuharibika wakati wa kupeleka Gharani kwa kutozingatia utaratibu sahihi uwekaji kwenye magunia na kutopepetwa vizuri.
Kwa upande wake mratibu wa mpango wa utafiti wa ufuta kitaifa na mtafifiti wa zao la ufuta kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) Naliendele Joseph Mzunda amesema kuwa kutokana na mnada uliofanyika hivi karibuni mkoani Songwe bei ya ufuta kwa kilo moja imeuzwa shilingi elfu 4,500 na kusema kuwa kunauwezekano wa bei kuendelea kupanda .
Sambamba na hilo amewaomba wakulima zao hilo kuuza katika mfumo unaoeleweka pamoja na kufuata taratibu sahihi za uvunaji na utunzaji wake kabla ya kupeleka sokoni.
Dr Fortunus Kapinga mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa kilimo ( TARI) Naliendele akionesha ufuta unaotakiwa usio takiwa na unao takiwa kuvunwa ukiwa shambani.