Jamii FM

Kipindi: Taka za plastiki chanzo kikuu mabadiliko ya tabianchi

8 June 2025, 10:09 am

Maafisa wa Mazingira kutoka Baraza la uhifadhi na utunzaji wa Mazingira NEMC kanda ya kusini wakiwa katika studio za jamii fm redio wakitoa Elimu ya athari zitokanazo na athari za taka za plastiki

Haya yalikuwa mahojiaono ya moja kwa moja studio na maafisa wa Mazingira kutoka Baraza la uhifadhi na utunzaji wa Mazingira NEMC kanda ya kusini siku ya june 5,2025 ikiwa ni siku ya Mazingira Duniani.

Na Musa Mtepa

Dunia inaendelea kuathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na taka za plastiki, hasa katika maeneo ya vizalia vya viumbe wa baharini, ikiwemo samaki.

Hayo yameelezwa June 5,2025 na Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kusini, Bw. Maguri Wambura, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii FM Radio.

Bw. Wambura amesema kuwa changamoto ya plastiki haijaiathiri Tanzania pekee, bali ni tatizo la dunia nzima kutokana na uzalishaji na matumizi makubwa ya bidhaa zitokanazo na plastiki.

Sauti ya 1 Maguri Wambura afisa mazingira Mwandamizi (NEMC) kanda ya kusini

Akizungumzia kuhusu katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki, Bw. Wambura ameeleza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa sheria, ambapo serikali ilianzisha matumizi ya mifuko mbadala ili kupunguza athari za kimazingira.

Sauti ya2  Maguri Wambura afisa mazingira Mwandamizi (NEMC) kanda ya kusini

Kwa upande wake, Mhandisi Msafiri Laurent kutoka NEMC Kanda ya Kusini, amesema kuwa taka za plastiki zimesababisha athari mbalimbali ikiwemo za kiafya, kiuchumi na kimazingira.

Sauti ya Mhandisi Msafiri Laurent kutoka NEMC kanda ya kusini

Katika kipindi hicho, baadhi ya wasikilizaji walioshiriki kwa njia ya simu waliitaka NEMC kuzuia uzalishaji wa plastiki viwandani badala ya kuzuia matumizi kwa watumiaji wa kawaida. Vilevile, wameomba elimu zaidi itolewe hasa katika maeneo ya vijijini ili jamii ielimike juu ya namna sahihi ya kutupa taka za plastiki ili kuepusha madhara kwa mazingira na afya ya jamii kwa ujumla.

Sauti ya Wasikilizaji(Wachangiaji kwa njia ya Simu)